Vikosi vya dharura vyaendelea kuwasaka manusura, Libya
15 Septemba 2023Umoja wa Mataifa umeyataja mafuriko hayo kuwa "janga" na umetoa wito wa zaidi ya dola milioni 71 ili kusaidia zaidi ya watu 250,000 kati ya 884,000 wanaoorodeshwa kuwa na uhitaji mkubwa.
Muuguzi Mona Talib Khaled amesema "Tunajitolea kuwaokoa ndugu zetu katika mji wa Derna, na kwa msaada wa Mungu, tutajitahidi na kuwaleta ndugu zetu kwenye maeneo salama. Mtu anapoona janga kama hili, kama binadamu lazima ahisi uchungu wa ndugu zake. Mtu yeyote anaweza kujitolea badala tu ya kubaki nyumbani."
Shirika la Hilali Nyekundu la Libya limesema watu 11,300 wamepoteza maisha na wengine 10,100 hawajulikani waliko.
Kimbunga Daniel kimeua watu 170 katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
Waziri wa afya wa serikali ya mashariki mwa Libya Othman Abduljaleel ameeleza kuwa, watu waliopoteza maisha wamezikwa kwenye makaburi ya halaiki nje ya mji ya Derna na miji mengine ya karibu.