Magazetini: Kuanza kambi za kuwahifadhi wakimbizi Bavaria
2 Agosti 2018Mhariri wa gazeti la Frankenpost anaandika kuhusu kambi za kuwahifadhi wakimbizi: Mhariri anaandika:
"Kambi za kuwahifadhi wakimbizi zimekwisha andaliwa kutokana na mbinyo wa chama cha CSU, hii ikiwa ni hofu ya wazi kutokana na uchaguzi wa jimbo la Bayern hapo Oktoba 14 bila kupoteza wingi wake. Chama hicho kinakabiliwa na hasira ya umma kuhusu mtazamo usiokubalika dhidi ya kile kinachojulikana kama wahamiaji wa kiuchumi. Chama cha CSU kimepitwa na katika uchunguzi wa maoni ya wapiga kura na kundi la wenye siasa kali za mrengo wa kulia, ambao wanataka kuchukuan hatua kali zaidi. Na kwa bahati mbaya wananchi wanaunga mkono msimamo huo mkali. Na sasa chama cha CSU kinataka kuchanganya masuala ya kidini na kijamii katika suala hili. Suala hilo halijapatiwa suluhisho, watu ambao hawatapatiwa haki ya hifadhi hapa nchini watalazimika kurejeshwa makwao. Mhariri anaandika kwamba , makambi ya kuwahifadhi wakimbizi yanahatari ya kugeuka kuwa eneo la mabanda."
Mhariri wa gazeti la Rhein-Zeitung la mjini Koblenz anazungumzia pia kuhusu kuanzishwa kwa makambi ya kuwahifadhi wakimbizi jimboni Bavaria. Mhariri anaandika:
"Mawaziri wakuu wa CDU na SPD walikutana , wakati walipokuwa wakijadili makubaliano yao ya kuunda serikali ya mseto. Kwa pamoja walisema kwamba wazo la kuwa na makambi ya kuwahifadhi wakimbizi si jambo zuri. Imani ya waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer kutoka chama cha CSU kwamba majimbo mengine huenda yatafuata nyayo za jimbo lake hazina msingi. Ni jimbo moja tu la Saxony lililokubaliana na wazo hilo. Chama cha CSU hata hivyo kimejizuwia kufanya sherehe kuhusiana na tukio hilo la kufunguliwa kwa vituo saba vya kuwahifadhi wakimbizi. lakini pamoja na hayo chama hicho kimegundua katika kampeni za uchaguzi kwamba hatua yao hiyo haijawaletei tija."
Kuhusu suala la uhalifu wa kupangilia, mhariri wa gazeti la Wiesbadener kurier anaandika kwamba Mwezi Mei 1990 , karibu miaka 28 iliyopita , ulitolewa ufafanuzi kuhusu kazi, kwa mtazamo wa polisi na mahakama suala la uhalifu wa kupangilia unawekwa wapi. Mhariri anaadika:
"Je ufafanuzi juu ya kazi unabeba mtazamo sawa kati ya kizazi kilichopita cha uhalifu na hii leo ? Nani ana haki ya kuuliza , iwapo ufafanuzi huo wa kazi wa wakati huo hauendani na uhalifu wa wakati huu , kuhusu kitisho na uwezo wa kuleta madhara kupitia makundi yanayojitokeza , ambayo sehemu zao za kazi zinaelezwa kama katika mtandao wa internet. Ili kwa maslahi ya umma iwezekane kupambana na makundi kama hayo!"
Naye mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung akizungumzia mada hiyo anaandika:
"Nchini Ujerumani hakuna nafasi kwa makundi ya uhalifu wa kupangilia, amesema waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer. wakati huo huo mwanasiasa huyo kutoka chama cha CSU anasema , makundi ya uhalifu wa kupangilia yantishia taifa na uchumi wa nchi. Nini maana ya kitisho kwa hiyo? Mbinu nyingi zimetumika lakini kila wakati kunaongezeka uhalifu wa kusafirisha watu au makundi ya kimafia. Hakuna sababu ya msingi , katika umma ulio katika jamii huru , ambapo makundi hayo ya kihalifu yanaweza kufaidika, na bila shaka yanapungua. Lakini pia hakuna sababu ya kubweteka na kujaribu kuyatetea makundi kama hayo kupitia mahakama ya katiba."
Mhariri wa gazeti la Westfalenpost anazungumzia kuhusu juhudi za kampeni inayojulikana kama Me Two na hali ya ubaguzi ya kila siku. Mhariri anaandika:
"Ni wakati muafaka , sasa wa kubadilisha mfumo na kuanza kusikiliza. Kwa mfano , mtu ambaye anakabiliwa na ubaguzi hata mdogo tu na haaminiki, kwamba amekabiliwa na hali hiyo. Hii ni pamoja na ukosoaji kuhusu kuishi pamoja, ni vizuri kuliangalia upya suala hilo. Kwamba iwapo mtu anapenda kula nyama ya nguruwe ama hapendi, si suala la kujadiliwa hapa, kwamba yeye ni Mjerumani safi. Katiba haina uhusiano na suala hilo. Sheria inakwenda kwa kila mtu, ambae anataka kuishi katika nchi yetu. Tunapaswa kuliangalia vizuri suala hilo."
Hayo ndio maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo kama yalivyokusanywa na Sekione Kitojo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Josephat Charo.