1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi yafutwa Romania

6 Desemba 2024

Mahakama ya Katiba ya Romania imeyafuta matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo, ambayo mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia Călin Georgescu alikuwa ameshinda.

https://p.dw.com/p/4nrIr
Uchaguzi Romania
Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi yafutwa RomaniaPicha: Bogdan Buda/AP/picture alliance

Waziri Mkuu Marcel Ciolacu amesema uamuzi wa mahakama hiyo ya katiba ni “uamuzi pekee sahihi” baada ya nyaraka za siri kuonyesha kwamba uchaguzi huo uliingiliwa na Urusi.

Hata hivyo mgombea wa urais anayefuata siasa za wastani Elena Lasconi ameukosoa vikali uamuzi huo.

Mgombea wa mrengo wa kulia aongoza uchaguzi wa Romania

Lasconi amesema zoezi la upigaji kura lilipaswa kuendelea ili kuheshimu sauti na matakwa ya wananchi wa Romania.

Duru ya pili ya uchaguzi huo wa urais ilitarajiwa kufanyika mnamo siku ya Jumapili.