1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Mahakama ya ECOWAS yaamuru Bazoum wa Niger kuachiwa

15 Desemba 2023

Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imeamuru kuachiliwa huru mara moja kwa rais wa Niger aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, ambaye amekuwa kizuizini tangu mapinduzi ya Julai 26.

https://p.dw.com/p/4aDy6
Mohammed Bazoum (kulia)
Kiongozi aliyepinduliwa mwezi Julai 2023 nchini Niger, Mohammed Bazoum (kulia)Picha: Presidency of Niger/AA/picture alliance

Kulingana na jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, mahakama ya ECOWAS imehimiza kuachiliwa bila masharti kwa Bazoum na pia imeamuru arudishwe mamlakani.

Niger imesimamishwa uanachama wa ECOWAS baada ya walinzi wa rais kumpindua Bazoum na kumuweka kizuizini pamoja na familia yake.

Uamuzi wa mahakama ya ECOWAS umeongeza kuwa, Mohamed Bazoum anasalia kuwa rais halali wa Niger.

Utawala wa kijeshi wa Niger haujatoa tamko lolote juu ya uamuzi huo wa mahakama. Hapo awali nchi nyingine wanachama wa ECOWAS, pia zimewahi kupuuza mahakama hiyo ya kikanda.