Mahakama ya ICJ yasikiliza kesi ya mabadiliko ya tabia nchi
3 Desemba 2024Matangazo
Mataifa madogo ya visiwa yanapeleka kilio chao mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa ya haki - ICJ kuhusiana na athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi wanazohisi zinatishia uhai wa visiwa hivyo.
Wanataka mataifa makubwa yanayochafua mazingira yabebeshwe jukumu. Mwaka jana Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliomba mahakama hiyo ya kusuluhisha migogoro ya Kimataifa, kutowa msimamo wake kuhusu wajibu wa mataifa ya ulimwengu kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi.
COP29: Makundi yatoka kwenye ukumbi wa mazungumzo kwa hasira
Hatua hiyo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ilikuja kufuatia miaka kadhaa, ya mataifa ya visiwa yanayokhofia kutoweka, kulishawishi baraza hilo. Kesi hiyo itasikilizwa kwa muda wa wiki mbili.