1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Mahakama ya ICJ kusikiliza kesi ya mateso inayoikabili Syria

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Kesi hiyo inasikilizwa siku ya Jumanne ambapo Syria inakabiliwa na madai katika mahakama hiyo kwamba inaendeleza mfumo wa mateso ambao umewaua maalfu ya watu.

https://p.dw.com/p/4XLHi
Canada na Uholanzi zimeiomba mahakama ya ICJ kwa haraka iitake Syria ikomeshe mateso yote na tabia ya kuwashikilia watu bila kuwafungulia mashitaka
Canada na Uholanzi zimeiomba mahakama ya ICJ kwa haraka iitake Syria ikomeshe mateso yote na tabia ya kuwashikilia watu bila kuwafungulia mashitakaPicha: Yves Herman/REUTERS

Kesi hiyo katika mahakama ya ICJ ni ya kwanza kwa Syria kuwakabili majaji wa kimataifa kuhusiana na vita vya kinyama vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2011.

Serikali ya Syria mjini Damascus imeitupilia mbali kesi hiyo ikiitaja kuwa habari potofu na uongo na kwamba madai hayo hayakidhi vigezo vya kuaminika.

Canada na Uholanzi zimeiomba mahakama ya ICJ kwa haraka iitake Syria ikomeshe mateso yote na tabia ya kuwashikilia watu bila kuwafungulia mashitaka.

Aidha iruhusu wachunguzi wa nje waingie katika magereza na itoe taarifa kwa familia kuhusu hatima ya wapendwa wao.

Kesi ya Jumanne ilikuwa isikilizwe kwa mara ya kwanza mwezi Julai lakini Syria iliiahirisha.