1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Mahakama ya ICJ, kusikiliza mzozo wa Armenia na Azerbaijan

12 Oktoba 2023

Armenia na Azerbaijan wamekabiliana katika mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa kuhusu mvutano wa Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4XRRT
Kesi hizi zinasikilizwa wiki chache baada ya Azerbaijan kufanya mashambulizi makali na kulirejesha kikamilifu mikononi mwake eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh. (Picha ya maktaba)
Kesi hizi zinasikilizwa wiki chache baada ya Azerbaijan kufanya mashambulizi makali na kulirejesha kikamilifu mikononi mwake eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh. (Picha ya maktaba)Picha: Wiebe Kiestra/UN

Yerevan imewataka majaji wa mahakama hiyo kuilazimisha Baku kuondoa wanajeshi kutoka Nagorno-Karabakh na kuwaruhusu Waarmenia waliofukuzwa makwao kurejea usalama katika eneo hilo lililojitenga.

Kesi hizi zinasikilizwa wiki chache baada ya Azerbaijan kufanya mashambulizi makali na kulirejesha kikamilifu mikononi mwake eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh kwa mara ya kwanza katika miongo mitatu na kusababisha Waarmenia wanaokadiriwa kufikia 120,000 waliokuwa wakiishi katika eneo hilo kukikimbilia Armenia.

Hii ni kesi ya karibuni zaidi kusikilizwa na ICJ katika mivutano ya kisheria iliyodumu kwa muda mrefu kati ya mahasimu hao wawili wanaoshutumiana kwa kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi wa Rangi (ICERD).