ICJ kuamua juu ya mamlaka ya kusikiliza kesi dhidi ya Urusi
29 Januari 2024Ukraine imedai Urusi ilitumia tuhuma za uwongo ikiisingizia kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wanaozungumza Kirusi wanaoishi Ukraine, kama sababu ya kuivamia nchi hiyo mwaka 2022.
Urusi kwa upande wake ilikataa kufika mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa ya Haki, ICJ mnamo mwaka 2022 na badala yake ikafungua kesi ya kupinga mamlaka ya mahakama hiyo.
Aidha siku ya Jumatano mahakama hiyo pia itatoa uamuzi wake katika kesi nyingine tofauti kuhusu mgogoro wa nchi hizo mbili, ambapo Ukraine inaitaka mahakama hiyo iiamrishe Urusi ilipe fidia kwa uhalifu na mashambulio iliyoyafanya dhidi ya jimbo la Crimea.
Ukraine ilifungua kesi mwaka 2017 ikiishtaki Urusi kwa madai ya kuzibagua baadhi ya jamii katika rasi ya Crimea baada ya kulinyakua eneo hilo.