Migogoro
Mahakama Israel yataka wafanyakazi kusitisha mgomo mara moja
2 Septemba 2024Matangazo
Mahakama ya kazi nchini Israel imeagiza kusimamishwa kwa mgomo wa nchi nzima ulioitishwa na chama cha wafanyakazi, wanaoishinikiza serikali kufikia makubaliano ya kuachiliwa mateka wanaoshikiliwa Gaza.
Hukumu ya mahakama hiyo ya Tel Aviv aidha imesema mgomo huo umechochewa kisiasa.
Somam pia:Waisraeli waanzisha mgomo wakishinikiza kuachiliwa kwa mateka
Hukumu hiyo imetolewa baada ya Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich anayepinga makubaliano katika vita kati yao na Hamas, kuiomba mahakama kuuzuia mgomo huo.
Mahakama hiyo imesema mgomo huo haukuitishwa kwa sababu za kiuchumi, na shirikisho hilo linaruhusiwa kuitisha migomo kwa sababu za kiuchumi na haki za wafanyakazi na si za kisiasa.