1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKenya

Mahakama ya Juu Kenya yaidhinisha sheria ya fedha, 2023

8 Septemba 2023

Mahakama ya Juu nchini Kenya hii leo imeidhinisha uamuzi uliotolewa mwezi Julai na mahakama ya rufaa kuthibitisha sheria ya fedha ya mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4W6kt
Kenia wartet mit Spannung auf das Urteil des Obersten Gerichtshofs zu den Wahlen
Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Sheria hiyo inalenga kuongeza maradufu kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa za mafuta. Aidha inaongeza tozo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa nyumba.

Sheria hiyo iliyoanza kutekelezwa Julai 28 , ilisababisha ghadhabu zilizofuatiwa na maandamano ya kupinga ugumu wa maisha nchini Kenya katika mwezi huo wa Julai.

Serikali ya Rais William Ruto imesema kodi za juu ni muhimu katika kusaidia kukabili ongezeko la deni na kufadhili mipango ya kubuni nafasi za ajira.