Mahakama ya Juu ya Ufaransa kuamua hatima sheria ya uhamiaji
25 Januari 2024Mswada huo ni mpango wa mageuzi muhimu ya muhula wa pili wa Rais Emmanuel Macron, lakini maandishi yake yalisababisha upinzani kutoka kwa wabunge wa chama tawala.
Vyama vya wafanyakazi na mashirika ya haki za binaadamu yaliitisha maandamano mapya siku ya Alkhamis (Januari 25), baada ya maelfu ya watu kumiminika mitaani kote Ufaransa mwishoni mwa wiki.
Soma zaidi: Macron na Le Pen washambuliana katika mdahalo
Macron aliwasilisha muswada huo kwa Baraza la Kikatiba kwa ajili ya kuutathmini.
Lakini pia aliutetea mswada huo, akisema ulihitajika ili kupunguza uhamiaji haramu na kuwezesha ujumuishaji wa wahamiaji waliopewa vibali.
Baraza hilo lina mamlaka ya kuondoa baadhi ya vipengele au kuufuta muswada wote kama litaona unakiuka katiba.
Mswada huo unafanya kuwa vigumu zaidi kuunganishwa kwa familia na kupatikana kwa mafao ya kijamii, na unajumuisha masharti kwa wafungwa wa uraia pacha kupokonywa uraia wao wa Ufaransa.