Mahakama ya katiba Ujerumani yasikiliza kesi dhidi ya NPD
4 Julai 2023Chama cha National Democratic,NPD kimekataa kushiriki kwenye mchakato huo kikidai kwamba hakina matarajio ya kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya haki.
Kwa mujibu wa naibu rais wa mahakama hiyo ya katiba, Doris König,hakuna ulazima wa chama hicho kuwepo mahakamani na kwamba mchakato wa kusikiliza kesi hiyo utafanyika bila ya chama hicho kushiriki.
Soma pia: Kesi ya NPD dhidi ya rais wa Ujerumani
Ni mara ya kwanza kwa mahakama ya Karlssruhe tangu ilipoanzishwa mwaka 1951 kuendesha kesi kuhusu uwezekano wa kukatiwa ufadhili wa kifedha chama cha kisiasa kwa kushukiwa kuwa na misimamo ya kuipinga katiba.
Chama cha NPD ambacho hivi sasa kinajiita chama cha Nyumbani kimesema kupitia tovuti yake kwamba hakitokubali kuwa watazamaji katika kile ilichokiita,mchakato wa kisheria.
Hata hivyo wanasiasa wa ngazi za juu nchini Ujerumani wanaitazama hatua ya chama hicho kususia kikao cha mahakama kama ishara ya wazi ya msimamo wake wa kupingana na katiba.