1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kenya yaamuru Meta kufunguliwa mshtaka

21 Septemba 2024

Mahakama nchini Kenya imeamua kwamba kampuni kubwa ya mtandao ya kijamii ya Marekani, Meta, inaweza kufunguliwa mashtaka kuhusu mazingira duni ya kazi na kuachishwa kazi kwa wafanyakazi wake.

https://p.dw.com/p/4kvaB
Mitandao ya kijamii
Mahakama nchini Kenya imeamua kwamba kampuni kubwa ya mtandao ya kijamii ya Marekani, Meta, inaweza kufunguliwa mashtaka kuhusu mazingira duni ya kazi na kuachishwa kazi kwa wafanyakaziPicha: Jonathan Raa/NurPhoto/picture alliance

Mahakama nchini Kenya imeamua kwamba kampuni kubwa ya mtandao ya kijamii ya Marekani, Meta, inaweza kufunguliwa mashtaka kuhusu mazingira duni ya kazi na kuachishwa kazi kwa wafanyakazi wake hatua inayofungua njia ya mapambano wa kisheria na wafanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo.

Uamuzi huo uliotolewa mjini Nairobi mnamo siku ya Ijumaa unafuatia kutimuliwa kazini kwa wasimamizi wa maudhui kwenye mtandao wa Facebook na kampuni ya SAMA iliyopewa kandarasi ya kusimamia kazi za kampuni ya Meta nchini Kenya. 

Soma zaidi. Wakenya waliotoweka waachiwa huku mashirika ya haki yakivilaumu vikosi vya usalama

Kesi ya kwanza iliwasilishwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na Daniel Motaung, msimamizi wa maudhui wa Afrika Kusini ambaye alifanya kazi katika kampuni hiyo.

Kesi nyingine iliyofunguliwa mwezi Machi mwaka jana, ambapo wasimamizi 185 waliofukuzwa kazi na Sama wanadai kuwa walizuiwa kutuma maombi ya majukumu sawa katika kampuni nyingine. Hata hivyo kampuni ya Meta ambayo mpaka sasa haijatoa tamko lolote bado inaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Juu.