Mahakama ya Kimataifa yaiamuru Syria kusitisha mateso
17 Novemba 2023Matangazo
Uamuzi huo umetolewa katika kesi ya kwanza ya kimataifa inayohusu vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza nchini Syria mwaka 2011.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki imeeleza kuwa taifa hilo linapaswa kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wake kuzuia vitendo vya utesaji na ukatili wa aina nyingine na adhabu zisizo za kiutu.
Ufaransa yatangaza hati ya kukamatwa kwa Rais wa Syria Assad
Imeamua pia kwamba, ni lazima Syria izuie uharibifu na ihakikishe inahifadhi ushahidi wa aina yoyote unaohusu mpango huo wa mateso.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Ufaransa kutoa waranti wa kukamatwa kwa rais wa Syria Bashar AL-assad anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kibinadamu kutokana na mashambulizi ya kemikali ya mnamo mwaka 2013.