SiasaAsia
Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo
9 Februari 2024Matangazo
Onyo hilo lilitolewa masaa 10 baada ya kufungwa kwa vituo vya uchaguzi.
Mmoja ya maafisa maalumu kwenye Tume ya Uchaguzi ya Pakistan (ECP), Zafar Iqbal, amesema baada ya kutangaza matokeo ya kwanza ya majimbo masaa 10 baada ya uchaguzi, changamoto ya mtandao ndio imesababisha kuchelewa huko.
Soma zaidi: Pakistan yaanza kuhesabu kura baada ya uchaguzi kukamilika
Ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya wagombea wanaoungwa mkono na waziri mkuu wa zamani aliyeko gerezani, Imran Khan, na chama cha Pakistan Muslim League ambacho pia ni cha waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif.
Picha halisi ya matokeo inatarajiwa kuanza kujitokeza leo Ijumaa (Februari 9) baada ya zoezi la kuhesabu kuendelea usiku kucha.