Kesi dhidi ya kampuni ya Total Energies yatupiliwa mbali
28 Februari 2023Mashirika hayo sita yasiyo ya kiserikali yanahoji kuwa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki - EACOP haukutimiza kile kinachofahamika kama wajibu wa uangalifu, ambao unayahitaji makampuni kuepusha madhara makubwa kwa haki za binaadamu, afya, usalama na mazingira. Mahakama hiyo ya mjini Paris imeamua kuwa kesi hiyo haikubaliki, ikisema kuwa walalamikaji hawakufuata taratibu za mahakama ipasavyo.
Mahakama ya raia mjini Paris itatoa uamuzi wake kuhusu kesi iliyowasilishwa na Shirika la Friends of Earth France na mashirika mengine matano ya waharakati kutoka Ufaransa na Uganda yanayoituhumu TotalEnergies kwa kunyakua ardhi ya zaidi ya watu 100,000 bila fidia ya kutosha na kuchimba mafuta kwenye hifadhi asili yenye viumbe na mimea iliyo hatarini kutoweka.