Matangazo
Baada ya mwili wa meneja wa teknolojia na mawasiliano wa tume inayosimamia uchaguzi Kenya IEBC Chris Musando kupatikana, siku tatu tu baada ya afisa huyo kutoweka, serikali imechukua hatua ya kuimarisha usalama wa mwenyekiti wa tume hiyo kwa kumpa askari w aziada. Mwili wa meneja huyo ulipatikana ukiwa na majeraha, katika hifadhi ya maiti jijini Nairobi. Hata hivyo tume yenyewe inasema haijaarifiwa kuhusu hilo. Mtangazaji Lillian Mtono amezungumza na makamu mwenyekiti wa IEBC, Connie Nkatha Maina anayeanza kwa kuzungumzia kifo hicho.