1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majadiliano ya mabadiliko ya tabia nchi , wajumbe washindwa kuafikiana

11 Desemba 2011

Awamu ya kufunga majadiliano ya Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi mjini Durban yameendelea kwa usiku wa pili huku kukiwa na mivutano.

https://p.dw.com/p/13QdK
South Africa's foreign minister Maite Nkoana-Mashabane speaks during a media briefing at the climate change conference taking place in the city of Durban, South Africa, Friday, Dec 9, 2011. The United States, China and India could scuttle attempts to save the only treaty governing global warming, Europe's top negotiator said Friday hours before a 194-nation U.N. climate conference was to close. (Foto:Schalk van Zuydam/AP/dapd)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika kusini Maite Nkoana-MashabanePicha: dapd

Wajumbe wakiwa na uchovu na Afrika Kusini ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo, ikisema kuwa matokeo ya kuaminika bado yanakaribia. Waziri wa mambo ya kigeni Maite Nkoana-Mashabane amesema, hatua za majadiliano zilizoanzia mjini Kyoto mwaka 1997 hazitahimili kushindwa tena kama ilivyotokea mjini Copenhagen miaka miwili iliyopita. Mataifa mengi , ikiwa ni pamoja na mataifa madogo ya visiwani yanayokabiliwa na kupanda kwa kiwango cha bahari, pamoja na Brazil na Afrika Kusini , zimekusanya nguvu zao katika mpango wa Umoja wa Ulaya. Mpango huo unatarajiwa kurefusha mkataba wa Kyoto na kulazimisha upunguzaji wa gesi za kaboni zinazosababisha uharibifu wa mazingira na kuleta ujoto. Lakini mataifa matatu ambayo ni watoaji wakubwa wa gesi hizo, Marekani, China na India yamekataa hadi sasa maelezo ya kulazimisha kisheria, hususan Marekani , ambako wahafidhina katika baraza la Congress wanapinga suala la kukaripiwa. Mswada wa Umoja wa Ulaya unaeleza kuwa awamu ya pili ya mkataba wa Kyoto unapaswa kumalizika mwishoni mwa mwaka 2017. Marekani inataka wachafuzi wote kuwekwa katika kiwango sawa cha sheria kuhusiana na upunguzaji wa gesi zinazoharibu mazingira, lakini China na India zinataka kuhakikisha uchumi wao unaendelea kukua bila ya kuwekewa vizingiti.