1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Majeshi ya Ufaransa kuondoka Burkina Faso baada ya siku 30

26 Januari 2023

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imesema leo kwamba itayaondoa majeshi yake yaliyopelekwa kusaidia kupambana na wanamgambo wa itikadi kali nchini Burkina Faso baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

https://p.dw.com/p/4MioO
Afrika Militär Missionen von Barkhane in Mali
Picha: Etat-major des armées / France

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imesema leo kwamba itayaondoa majeshi yake yaliyopelekwa kusaidia kupambana na wanamgambo wa itikadi kali nchini Burkina Faso baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa. Hatua hiyo inafuatia shinikizo kutoka kwa serikali ya kijeshi, na inayofanana na ile iliyochukuliwa na taifa jirani, Mali.

Afisa wa ngazi za juu kwenye wizara hiyo amesema Ufaransa imearifiwa rasmi na serikali ya Burkina Faso uamuzi wa kusitisha makubaliano ya mwaka 2018 yanayohusu kuwepo kwa majeshi ya Ufaransa nchini humo.

Kiasi wanajeshi 400 wa vikosi maalumu wako Burkina Faso, ikiwa ni sehemu ya wanajeshi 3,000 walilopelekwa nchini humo kukabiliana na wanamgambo hao wa itikadi kali katika ukanda wa Sahel, barani Afrika.

Katika hatua nyingine, wizara hiyo ya mambo ya nje imesema itamuita balozi wake ikirejelea muktadha wa hali ilivyo kwa sasa, siku moja baada ya kutangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini humo.