SiasaUrusi
Urusi yashambulia kusini mwa Odesa, Ukraine
17 Septemba 2023Matangazo
Jeshi la anga la Ukraine limesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba Urusi imefanya mashambulizi sita ya droni za Shahed zinazotengenezwa Iran pamoja na makombora 10.
Lakini jeshi la Ukraine lilifanikiwa kudungua droni sita na makombora sita kabla ya kuanguka kwenye maeneo yaliyolengwa.
Hali kwenye mkoa wa Odesa na bandari zake imekua ikifuatiliwa kwa karibu na wanunuzi wa nafaka baada ya Kyiv kusema jana Jumamosi kwamba meli zenye shehena za nafaka zimewasili mkoani humo zikitumia ujia wa muda kufika kwenye bandari za Bahari Nyeusi ili kuzisafirisha kuelekea Afrika na Asia.