Makubaliano ya Israel na Hamas hayatofanyika kabla ya Ijumaa
23 Novemba 2023Matangazo
Ripoti hiyo imeondowa matumaini ya jamaa za wanaoshikiliwa mateka, waliotarajia watu wao kuachiliwa leo Alhamisi. Jana Jumatano, Israel na kundi la Hamas walikubaliana kusitisha vita Gaza, kwa siku nne kupisha misaada ya kibinadamu pamoja na kuachiliwa huru kwa mateka wasiopungua 50 wanaoshikiliwa na Hamas, kwa kubadilishana na Wapalestina kiasi 150 waliofungwa katika jela za Israel.
Soma pia:Papa Francis akutana na jamaa za waliotekwa na Hamas na wafungwa wa Palestina
Taarifa zinasema mapigano yameshuhudiwa yakiendelea leo, huku utekelezaji wa makubaliano ya usitishaji vita ukisogezwa hadi kesho Ijumaa. Moshi mzito umeripotiwa kutanda katika anga ya eneo la vita la Kaskazini mwa Gaza.