1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya kijihadi ya Syria yaushambulia mji wa Aleppo

29 Novemba 2024

Makundi ya kijihadi na washirika wao wanaoungwa mkono na Uturuki wameshambulia kwa makombora mji wa Aleppo, wa pili kwa ukubwa nchini Syria

https://p.dw.com/p/4naj1
Syria
Makundi ya kijihadi ya Syria na washirika wake yashambulia mji wa AleppoPicha: Omar Albam/AP/picture alliance

Kulingana na shirika moja la kufuatlia vita nchini Syria, ghasia hizo zimesababisha vifo vya watu 255, wengi wao wakiwa wapiganaji wa pande zote mbili. Idadi hiyo pia inajumuisha raia 24, wengi waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Urusi.

Kulingana na Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria, kufikia leo Ijumaa, makundi hayo yalikuwa yameteka zaidi ya miji na vijiji 50 kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Syria, hatua kubwa ambayo imepigwa na makundi yanaoipinga serikali kwa miaka mingi.

Mamia ya watu wauawa katika mapigano ya waasi na jeshi nchini Syria

Afisa mmoja wa usalama wa serikali ya Syria aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya kijeshi vimewasili mjini Aleppo na akaongeza kuwa kuna vita vikali na mapigano magharibi mwa Aleppo, lakini ghasia hiyo hazijaenea hadi mjini .