Malema achaguliwa tena kama kiongozi wa chama cha EFF
16 Desemba 2024Johannesburg
malema alikianzisha chama hicho miaka 11 iliyopita, huku akitolewa mwito wa kuweka pembeni tofauti zake na Jacob Zuma wa chama cha uMkhonto weSizwe.
Malema amechaguliwa tena kuwa rais wa chama hicho, huku watu waliokuwa wa karibu yake ndani ya chama hicho tangu kilipoanzishwa, wakiwa wamemkimbia na kuungana na chama cha uMkhonto weSizwe, hali ambayo wachambuzi wa siasa wanadai inaashiria kuporomoka taratibu kwa EFF.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama hicho walikutana mjini Johannesburg tangu jumamosi wiki iliyopita, kumchagua rais wa chama, Makamu rais, Mwenyekiti mkuu wa chama kitaifa, Mweka Hazina Mkuu, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu.
Kupatikana kwa uongozi mpya wa EFF ni maandalizi ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, uliopangwa kufanyika nchini humo mwaka 2026.