Mali yasitisha makubaliano na Watuareg
26 Januari 2024Matangazo
Katika taarifa iliyosomwa kwenye runinga ya taifa, maafisa wa kijeshi wamesema haiwezekani tena kuendelea na makubaliano hayo kutokana na waasi hao kutotekeleza ahadi zao na "vitendo vya uadui" vinavyofanywa na mpatanishi mkuu Algeria.
Kutokana na hilo, utawala wa kijeshi umeeleza kuwa makubaliano ya amani yaliyojulikana kama Makubaliano ya Algiers, yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa umesitishwa.
Soma zaidi: Jeshi la Mali lawataka wakaazi wa Kidal wawe watulivu baada ya kuudhibiti mji huo
Serikali imetangaza mara moja usitishwaji mara moja wa makubaliano hayo.
Kundi la CMA ambalo ni muungano wa makundi ya waasi yaliyoundwa na jamii ya watu wa kuhamahama wa Toureg nchini Mali, limesema halikushangwa na uamuzi huo.