SiasaHaiti
Watu 1,500 wafa Haiti kutokana na vurugu za kihalifu
28 Machi 2024Matangazo
Kulingana na ripoti hiyo mamia ya watu walichomwa moto na magenge yanayodai kwamba yalikuwa yanajilinda.
Katika taarifa iliyotolewa leo pamoja na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya taifa hilo la Karibia, mkuu wa shirika hilo Volker Turk ametoa wito wa vitendo hivyo kukomeshwa mara moja.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu 4,451 waliuwawa mwaka jana huku hao zaidi ya 1,500 wakiwa wamefariki dunia kufikia Machi 22 huku machafuko yakizidi.
Machafuko ya Haiti yameshuhudia magenge yaliyojihami kuvamia vituo vya polisi na uwanja wa ndege wa kimataifa nchini humo. Waziri Mkuu Ariel Henry, alitangaza kujiuzulu mnamo Machi 11.