1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya watu wakusanyika kwa tamasha la ukumbusho Kenya

8 Julai 2024

Mamia ya Wakenya walikusanyika Jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi kwa tamasha la kuwakumbuka watu waliouawa kufuatia maandamano makali ya kupinga muswada tata wa fedha

https://p.dw.com/p/4hzNW
Kenia I Nationaler Streik gegen Steuererhöhungen
Picha: Tony Karumba/AFP

Watu walimiminika katika uwanja wa Uhuru Park katikati mwa Nairobi kuanzia saa sita mchana kusikiliza wasanii na kuwakumbuka waliofariki.

Umati mkubwa wa watu uliimba "Ruto lazima aende", wakirejelea matakwa yaliyotolewa nawaandamanaji katika wiki zilizopita, huku wakipeperusha bendera za Kenya na kucheza mbele ya waimbaji na wasanii.

Soma pia:Rais William Ruto wa Kenya aahidi mabadiliko baada ya maandamano

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema kuwa maandamano ya awali ya amani yaliyokuwa yakiongozwa na vijana maarufu kama Gen-Z yaligeuka kuwaghasia na kusababisha vifo vya watu 39.

Tamasha lafanyika siku ya Saba Saba

Tamasha hilo lilifanyika katika siku ya kile kinachoitwa "Saba Saba," siku ya saba ya mwezi wa saba, kuashiria wakati wa mwaka 1990 ambapo upinzani uliibuka kutaka kurejeshwa kwa demokrasia ya vyama vingi.