1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Mamilioni wajifungia majumbani Shanghai kufuatia kimbunga

16 Septemba 2024

Mamilioni ya watu katika mji wa Shanghai na maeneo mengine ya pwani ya Mashariki ya China wakumbwa na kimbunga Bebinca.

https://p.dw.com/p/4kfLa
China | Kimbunga Bebinca
Kimbunga Bebinca chawaathiri wakaazi wa ShangaiPicha: Hector Retamal/AFP/Getty Images

Mamilioni ya watu mjini Shanghai na katika maeneo mengine ya China yanayokaliwa na watu wengi ya pwani ya mashariki mwa nchi hiyo wamelazimika kujifungia majumbani mwao Jumatatu, kufuatia kimbunga kikali zaidi kuwahi kulikumba eneo hilo tangu mwaka 1949.

Kimbunga hicho kimesababisha miti kuanguka pamoja na kutatiza usafiri katika eneo zima.

Kimbunga Bebinca kilipiga asubuhi ya Jumatatu katika eneo la pwani ya mashariki ya Shanghai kikiandamana na upepo mkali uliovuma kwa kasi ya zaidi ya kilomita 151 kwa saa,kwa mujibu wa kituo cha serikali cha televisheni cha CCTV.

Wakaazi milioni 25 wa mji wa Shanghai walishauriwa wabakie majumbani mwao.Mvua kubwa imenyesha kufuatia kimbunga hicho huku shughuli za kibiashara zikiwa zimefungwa.