Raia wa Taiwan waanza kupiga kura kumchagua rais
13 Januari 2024Mamilioni ya wakaazi wa kisiwa cha Taiwan, wameanza zoezi la upigaji kura hii leo, katika uchaguzi wa rais na bunge ambao unafuatiliwa kwa ukaribu duniani kote.
Kiongozi atakayechaguliwa anatarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa kisiwa hicho cha kidemokrasia, kinachokabiliwa na ongezeko la uchokozi wa China. China inadai kuwa kisiwa hicho kinachojitawala, kuwa sehemu ya himaya yake na kwamba haitosita kutumia nguvu kuleta umoja.
Mgombea wa chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP)Lai Ching-te amejipambanua kuwa mlinzi wa demokrasia ya Taiwan. Mpinzani wake mkuu Hou Yu-ih anapigia upatu uhusiano na China.
Wagombea urais: Wafahamu wagombea wakuu watatu wa urais Taiwan
Matokeo ya uchaguzi wa leo yanatizamwa kwa karibu na mataifa mawili ya China na Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa kijeshi wa kisiwa hicho. Mataifa yote mawili yenye uchumi mkubwa yamekuwa yakipigania ushawishi katika eneo hilo muhimu la kimkakati.