1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANAMA: Kansela Schröder aendelea na ziara ya nchi za Ghuba

2 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaL

Kansela wa Ujerumani, Gerhard Schröder, amefika Bahrain, akiendelea na ziara yake katika nchi za eneo la Ghuba. Akiwa kwenye mji mkuu wa nchi hii, MANAMA, alikutana na waziri mkuu SALMAN AL KHALIFA.

Kansela Schröder ataweka jiwe la msingi kwenye jengo la chuo kikuu kinachojengwa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Hannover.

Kabla ya hapo, alipokuwa nchini Qatar, Kansela aliendelea kutafuta tenda kwa viwanda vya Ujerumani kwa kuzungumzia teknolojia ya magari moshi ya kisasa, Transrapid. Nchi za eneo la Ghuba zinafikiria kujenga reli ya urefu wa kilometa 800 itakayoziunganisha nchi zote.