1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester City hatimaye ni mabingwa wa Ulaya

11 Juni 2023

Jitihada za muda mrefu za kocha Pep Guardiola kushinda tena Ligi ya Mabingwa Ulaya zilifikia mwisho jana jusiku wakati Manchester City hatimaye walitwaa ubingwa wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4SRXd
UEFA Champions League | Finale | Manchester City vs Inter Mailand
Picha: JON OLAV NESVOLD/Bildbyran/IMAGO

Mara ya mwisho Guardiola alibeba Kombe la Ulaya miaka 12 iliyopita timu yake ya Barcelona ilionyesha mchezo bora kabisa na kuisambaratisha Manchester United kwa mabao 3 -1 dimbani Wembley.

Soma pia: Manchester City na Inter Milan kumenyana leo kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa FA katika uwanja wa Ataturk Olympic mjini Istanbul.

Lakini jana usiku, ushindi mwembamba wa 1 - 0 dhidi ya Inter Milan mjini Instanbul hautakumbukwa kama mojawapo ya michezo bora zaidi waliowahi kucheza katika miaka saba tangu kocha huyo alipowasili mjini Manchester.

Lakini ulikuwa ndio muhimu zaidi kama klabu ambayo kwa muda mrefu imeishi kivulini mwa Manchester United na sasa imetoshana na mafanikio ya timu ya msimu wa 1998/99 kwa kushinda mataji matatu katika msimu mmoja ya Premier League, Kombe la FA na Champions League. Bao pekee na la ushindi la Man City lilifungwa na Rodri zikiwa zimesalia dakika 22 mchezo kumalizika.