Maoni : G20 – Ni kuhusu kujinusuru tu
9 Julai 2017Mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka huu huko Hamburg ungelikuwa mbaya zaidi kuliko vile ilivyokuwa.Sio tu fujo za mitaani za kihuni wala uharibifu uliokuwa ukizidi kuongezeka kwa kadri siku zilivyosonga mji huo wa bandari wa kaskazini ulikuwa kitovu cha kiwango cha matumizi ya nguvu,uharibifu na uporaji ambacho takriban hakijulikani kwa Wajerumani wengi.
Kilichotegemewa kuwa kibaya zaidi badala yake yalikuwa matokeo halisi yaliofikiwa na mataifa 19 na Umoja wa Ulaya yaliokuwa yakihudhuria mkutano huo wa kilele.Ile dhana tu ya wahusika wote kuketi kwa pamoja kukubaliana juu ya taarifa ya ufungaji wa mkutano huo ilikuwa inatosha kumtowa mtu kijasho chembamba.
Mezani tumeshuhudia watetezi wa demokrasia wakiketi meza moja pembezoni mwao wakiwa wataalamu wasomi hasa sio malaghai na pia kuna wavunjaji wa haki za binaadamu.Wengine wamevaa mashati meupe wakati wengine wakikabiliwa na madai ya rushwa.Halafu kuna kiumbe Donald Trump mtu anayependa kuchochea mvutano duniani na sera yake ya kulazimisha bila ya kutetereka ya "Marekani Kwanza."
Mafanikio
Kwa hiyo kwa kuzingatia mazingira mtu anabidi tu aridhike na matokeo yaliofikiwa katika mkutano huo wa kilele wa G20.
Cha kushangaza wahusika wote wamekubaliana kupambana na hatua za kuhami masoko wakati wakiendelea kutii taratibu zilizoainishwa na Shirika la Biashara Duniani.Huko ndiko hasa aina ya kujitolea kwa kuchukuliwa hatua kwa msimamo wa kimataifa ambapo angelipendelea Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.Kwa vyo vyote vile ni mafanikio yaliyotokana na yeye pongezi kwa hilo zimesikika kutoka kambi ya rais wa Ufaransa halikadhalika Urusi.
Hata hivyo katika suala la tabia nchi inamuwia mtu vigumu kuona hisia ya mafanikio au umoja.Marekani inajitowa rasmi katika Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na hili sasa liko wazi katika taarifa ya mkutano huo wa kilele.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya G20 kwamba uasi wa wazi umepita bila ya kuchuliwa hatua za kinidamu.
Kutofanikiwa
Hata hivyo siku kama hizi jambo hili sio zuri sana.Mapendekezo ya kuwawezesha wanawake,kugharamia miradi ya maendeleo ya Afrika na kukuza umahiri wa digitali ni ya kupongezwa sana lakini pia hayatoshi.
Mkutano wa kilele wa G20 umeshindwa kuupa utandawazi sura mpya inayohitajika mno.Mamilioni ya watu duniani wanaamini kwamba uchumi wa dunia unatumika tu kuwanufaisha wateuliwa wachache.
Mwishoni mwa mkutano huo wa kilele Merkel amesema maandamano yasio ya vurugu yameshawishi na kuchangia mazungumzo hayo ya siku mbili.Hata kama ni ukweli kulikuwa hakuna dalili ya maandamano hayo.
Kansela huyo wa Ujerumani alituhumiwa kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa G20 kwa kutaka kuutumia kuinadi taswira yake kiishara kama kiongozi wa dunia mwenye mafanikio kabla ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani uliopangwa kufanyika hapo mwezi wa Septemba.
Mwandishi :Dagmar Engel/Mohamed Dahman
Mhariri :Lilian Mtono