1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jee yatatekelezwa?

Admin.WagnerD24 Februari 2016

atika maoni yao wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya makubaliano ya kusimamisha mashambulio nchini Syria yaliyofikiwa baina ya Urusi na Marekani.

https://p.dw.com/p/1I11M
Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-AssadPicha: imago/ITAR-TASS

Mhariri wa gazeti la "Norwest"anasema licha ya makubalino hayo mashambulio yataendelea.Anasema walichokubaliana warusi na wamarekeni ni kuwadhibiti washirika wao katika kila upande.Lakini yapo makundi mengine ya kigaidi kama vile Al-Nusra na "dola la kiislamu" Mhariri wa "Nordwest" anaeleza kuwa makubaliano hayo hayawahusu magaidi hao.

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" linatilia maanani kwamba Rais Bashar Al-Asaad amekubali kusimamisha mapambano kutokana na shinikizo kutoka Urusi.Hayo yanaonyesha wazi kwamba Urusi inamdhibiti mbabe huyo wa Syria. Sababu ni kwamba majeshi yake hayatakuwa na nguvu bila ya msaada wa Urusi.

Gazeti la "Münchner Merkur " linesema makubalino ya kusimamisha mapambapano yangeliweza kutekelezwa nchini Syria laiti pande zinazopigana zingelikuwa mbili tu.

Anaeleza kuwa ziko pande tele. Mhariri wa "Münchner Merkur" anasema mbali na pande kuwa nyingi, pande hizo zina maslahi tofauti. Kwa mfano Uturuki inafikiria kwamba inayo haki ya kulipiza kisasi, sababu ambayo inaweza kutumiwa na kila upande. Hata hivyo, mhariri wa gazeti la"Münchner Merkur" anasema kwamba kusimamisha mapigano ni habari nzuri, na kwa hivyo litakuwa kosa ikiwa makubaliano yaliyofikiwa hayatatekelezwa.

Umasikini nchini Ujerumani
Umasikini nchini UjerumaniPicha: picture alliance/dpa/S. Pilick

Idadi ya masikini yaongezeka Ujerumani

Wahariri wa magezeti leo pia wanatoa maoni juu ya ripoti inayohusu umasikini nchini Ujerumani. Mhariri wa gazeti la Landeszeiotung" anasema ni jambo la kulitilia maanani kwamba asilimia 15 ya watu ni mskini nchini Ujerumani .

Mhariri huyo anakumbusha kwamba Ujerumani ni miongoni mwa nchi tajiri kabisa duniani. Anasema sababu ya umasikini huo ni ukweli kwamba ustawi wa uchumi hauna maana kwamba kila mwananchi ananufaika. Na anatahadharisha kuwa kiwango kikubwa cha umasikini kinaweza kuchochea machafuko ya kijamii.

Mhariri wa gazeti la "Mittelbayarische " anaiunga mkono tathmini hiyo. Anasema kwa miaka mingi sasa, ustawi wa uchumi umeacha kuchangia katika neema ya watu .Mwenendo huo unaandamana na hatari ya kuzuka ghasia.

Hali hiyo haikutokea kwa nasibu ,bali inatokana na sera tepetevu. Litakuwa jambo la munufaa kwa pande zote za jamii ikiwa pengo kati ya masikini na tajiri litazibwa. Suala hilo ni muhimu kwa mustakabal wa nchi na siyo porojo za kijamii.

Gazeti la "Thüringische" linaeleza kwamba umasikini nchini Ujerumani hauna maana kwamba mtu hana chakula.

Lakini ukweli ni kwamba vipato vya wafanyakazi vipo juu kidogo ya kipimo cha umasikini.

Ripoti juu ya umasikini nchini Ujerumani hailitilii maanani jambo hilo na wala haisemi kwamba tajiri wanazidi kuwa tajiri na masikini wanazidi kuwa masikini.

Mwandishi:Mtullya Abdu. Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Yusuf Saumu