Maoni:Tetemeko kujiuzulu Kramp-Karrenbauer halikutisa tu CDU
11 Februari 2020Kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama cha CDU Annegret Kramp-Karrenbauer na kujitoa kwake kuwa mgombea wa kiti cha kansela wa Ujerumani, ni kutokana na kutojiamini, katika chama ambacho kimeanza kukosa mwelekeo. Lakini tetemeko hilo linafika mbali.
Chama cha CDU kimejikwaa. chama kingine kikuu cha SPD, kwa muda mrefu sasa kinatafuta mwelekeo, kinatafuta kisimamie wapi, kinatafuta msingi wake. Kama ilivyokuwa kwa kiongozi wa chama cha SPD Andrea Nahles mapema katikati ya mwaka 2019 baada ya miezi 13 tangu kuingia katika uongozi wa chama hicho kikongwe nchini Ujerumani , sasa Kramp-Karrenbauer nae ametangaza kujiuzulu baada ya miezi 14 tu madarakani.
Nini kinachofuata baada ya hapa ? Majina, majina , majina, uvumi na matarajio. Lakini swali kuhusu nani atakiongoza chama hicho hapo baadaye na nani anaweza kuwa mgombea wa wadhifa wa kansela linaendelea kuwapo. Chama kinapaswa kuweka wazi kuhusu kujitambua pamoja na umoja wao.
Kwasababu kwa muda mrefu sasa CDU inaonekana kuwa si chama kilichokuwa pamoja , katika jimbo la Thuringia na Ujerumani kwa jumla , katika mitandao na kazi zake za kila siku, kwa kuwa kila mara kinaonekana kuwa na mivutano.
Wiki kumi na moja zimepita, baada ya mkutano wa kila mwaka wa chama cha CDU mjini Leipzig na kilimshangilia Kramp-Karrenbauer kuwa kiongozi wake, na baada ya ukosoaji mkubwa dhidi yake.
Ujerumani katika mwaka mmoja ujao inakabiliwa na uchaguzi mkuu.
Utakuwa uchaguzi utakaoamua sio tu kuhusu suala, la iwapo lakini pia ni vipi chama cha CDU na vyama vinavyounda serikali vitabakia katika uongozi ama vinaweza kubakia. Suala litakuwa kuhusu wabunge, umuhimu wa vyama, nidhamu ya chama pamoja na uhuru wa wabunge. Na mjadala ni kuhusu swali, iwapo na vipi vyama vya siasa za wastani vinaweza kupata nguvu na kupambana na vyama vile vinavyolemea siasa za kizalendo.
Sababu alizotoa Kramp-Karrenbauer kuhusiana na uamuzi wake uliokuja na kimbunga kikali kwa jamii, ni kwamba CDU yenye nguvu inahitaji uongozi imara. Hatimaye hali inahusu hali ya baadaye ya demokrasia nchini Ujerumani.
Karibu miaka 71 baada ya kuundwa jamhuri ya watu wa Ujerumani inaingia katika majaribu makubwa, pengine inawezekana ni mwanzo wa mwisho wa mfumo wake wa vyama. Suala lingine, ni kuhusu chama imara cha walinzi wa mazingira, cha kijani, kama kitaweza ama la kuchukua jukumu la vyama vya hivi sasa vikuu vya umma.