Mapigano nchini Syria yasababisha vifo vya watu 23
4 Septemba 2023Mkuu wa shirika hilo linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman, ameripoti kufariki dunia kwa watu 18 miongoni mwa kikosi kinachoiunga Uturuki na watano kutoka kikosi cha serikali ya Syria na kuongeza kuwa wengine walijeruhiwa.
Soma pia:Iran: Mashambulizi dhidi ya Syria huenda yakachochea visasi
Kulingana na shirika hilo linalotegemea mtandao mpana wa vyanzo nchini Syria lenye makazi yake nchini Uingereza, mapigano hayo yametokea Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Tal Tamr.
Kikosi cha SDF na washirika wake chafanya mashambulizi ya kisasi
Shirika hilo limeongeza kuwa kikosi kutoka kwa muungano wa makundi ya waasi yanayoungwa mkono na Uturuki, yanayojulikana kama Jeshi la Kitaifa la Syria yalitaka kujipenyeza katika eneo hilo mapema siku hiyo.
Soma pia:Maafisa wa Marekani watuliza hali ya mambo Deir al Zor
Shirika hilo limeendelea kusema kuwa jeshi la Syria na wapiganaji wa ndani wanaoshirikiana na Kikosi cha Kidemokrasia cha Syria (SDF) kinachoongozwa na Wakurdi, walijibu hatua hiyo na kusababisha majeruhi.
Uturuki imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Wakurdi Kaskazini mwa Syria
Eneo la Tal Tamr liko karibu na ukanda wa eneo la mpaka chini ya udhibiti wa Uturuki na washirika wake. Tangu mwaka 2016, Uturuki imefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya vikosi vya Wakurdi Kaskazini mwa Syria ambayo yameiwezesha Uturuki kuchukuwa udhibiti wa maeneo ya mpakani.
Mapema hapo jana Jumapili, ubalozi wa Marekani nchini Syria, ulisema kuwa maafisa wake wakuu walikutana na vikosi vinayoongozwa na Wakurdi pamoja na viongozi wa kijamii Mashariki mwa Syria kuzungumzia haja ya kupunguza mapigano hayo baada ya siku kadhaa za vurugu mbaya.
Viongozi wa Marekani wakutana na kikosi cha SDF
Ubalozi huo umesema kuwa naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Mashariki ya Karibu Ethan Goldrich pamoja na kamanda wa muungano unaoongozwa na Marekani unaopigana na kundi linalojiita dola la kiislamu IS nchini Syria na Iraq, meja jenerali Joel Vowell, walikutana Kaskazini Mashariki mwa Syria na kikosi cha SDF, mamlaka ya Wakurdi na viongozi wa kikabila jimboni Deir Ezzor.
Soma pia:Watu wenye silaha waua askari 23 Syria
Mkutano wakubaliana kuhusu umuhimu wa kushughullikia malalamiko ya wakazi wa Deir Ezzor
Taarifa ya ubalozi huo iliyochapishwa katika mtandao wa kijamii wa X ambao awali ukijulikana kama twitter, imesema kuwa walikubaliana kuhusu umuhimu wa kushughulikia malalamiko ya wakazi wa jimbo la Deir Ezzor, athari ya muingilio kutoka nje na haja ya kuepusha vifo vya raia pamoja na majeruhi. Washiriki wa mazungumzo hayo pia walikubaliana kuhusu haja ya kupunguzwa kwa vurugu haraka iwezekanavyo.