Mapigano makali yazuka kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23
10 Februari 2023Mapigano hayo yalitokea kilometa 8 kaskazini mwa mji wa Sake mkoani Kivu ya kaskazini.
Maelfu ya raia walilazimika kukimbia huku baadhi wakielekea mji wa Goma na wengine katika mkoa jirani wa kivu kusini.
Hali iliendelea kuwa ya wasiwasi mchana kutwa wa jana Alhamisi kwenye vijiji vya Kimoka na Luhonga vinavyoukaribia mji mdogo wa Sake ulioko umbali wa kilometa 27 magharibi mwa mji wa Goma, ambako maelfu ya raia walikimbia wakati jeshi la Congo lilikuwa likikabiliana na waasi wa M23.
Mkuu wa UNHCR ziarani Burundi kuwatembelea wahamiaji wa DRC
Wakizungumza na DW, raia hao baadhi ikiwa ni watoto na wanawake walilazimika kutembea kwa mguu kuelekea mjini Goma ambao umesalia mji pekee wa kukimbilia kwa maelfu ya raia wanaohangaishwa na vita hivyo.
Hadi Alhamisi jioni, wananchi wa Sake walionekana wakiwa wamepiga kambi kando na barabara wakiwa wamebeba mizigo na mifugo yao lakini bila matumaini ya kurudi tena majumbani kwao kutokana na milio ya risasi iliyoendelea kusikika kando na mji huo wa kimkakati wilayani masisi.
Mzozo wa Kongo wajadiliwa Bujumbura
Mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la congo,yameendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo mkoani kivu kaskazini licha ya kuwepo kwa mikutano ya viongozi wa kikanda jijini luanda na Nairobi ,kulitaka kundi hilo kuondoka katika maeneo yote linalodhibiti.
Hata hivyo, wabunge wa eneo hili wamelaani mapigano hayo huku wakilitaka jeshi kuwa na nidhanamu ambayo ni njia pekee ya kushindana na adui.
Papa Francis awataka Wakongo kusamehe
Mapigano hayo ya jana yanakuja baada ya waasi hao wa M23 kuuteka mji wa kimkakati wa kitshanga na kuongeza hofu kubwa kwa raia.