1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mapya yazuka kati ya M23 na wapiganaji hasimu DRC

30 Desemba 2022

Mapigano mapya yamezuka kati ya waasi wa M23 na wanamgambo hasimu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4LZXm
DR Kongo | kongolesische Soldaten auf dem Weg zur Front im Kampf gegen die M23-Rebellen
Picha: Arlette Bashizi/AFP/Getty Images

Duru za eneo hilo zimeeleza kuwa mapigano hayo yalizuka jana kwenye eneo la Tongo katika mji wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini.

Mwanaharakati wa asasi za kiraia, Safari Haguma, amesema milio ya risasi ilisikika kuanzia majira ya asubuhi.

Dominique Ndaruhutse, aliyejitangaza kuwa jenerali wa kundi la wanamgambo la CMS/FDP, pia amethibitisha kuhusu mapigano hayo na amesema wapiganaji 13 wa M23 wameuawa.

Jules Mulumba, msemaji wa muungano ya makundi yenye silaha ambao unalijumuisha kundi la CMS/FDP, amesema wameamua kupigana kuhakikisha nchi yao haiingiliwi kutoka nje, na kamwe hawatokubali kuwa watumwa.

Amesema kundi la M23 wana lengo la kusonga mbele kuelekea mji wa Kitshanga, ulioko umbali wa kilomita 125 magharibi mwa Goma.