SiasaSomalia
Mapigano yaibuka Jubaland nchini Somalia
11 Desemba 2024Matangazo
Ripoti kuhusu mapigano hayo imetolewa na Adan Ahmed Haji, ambaye ni naibu waziri wa usalama wa Jubaland ambaye amefanya mkutano wa waandishi habari katika mji mkuu wa jimbo hilo,Kismayu.
Mapigano hayo yanaonesha kutanuka kwa mivutano katika eneo hilo baada ya Jubbaland kufanya chaguzi zake kinyume na ushauri wa serikali kuu.
Mwishoni mwa mwezi Novemba jimbo hilo linalopakana na Kenya na Ethiopia lilimrudisha tena madarakani rais wake Ahmed Islam Madobe kwa muhula wa tatu.