Marekani kulegeza vikwazo vya mafuta dhidi ya Venezuela
19 Oktoba 2023Marekani imetangaza kuwa italegeza baadhi ya vikwazo vya mafuta na gesi dhidi ya Venezuela baada ya serikali ya nchi hiyo na upinzani kufikia makubaliano ya kufanya uchaguzi mwaka ujao. Wizara ya fedha ya Marekani imesema nafuu hiyo ya vikwazo inaweza kubadilika au kufutwa endapo Venezuela itashindwa kutekeleza makubaliano hayo.
Utawala wa Marekani chini ya Rais Joe Biden, ambaye kwa muda mrefu aliahidi msamaha wa vikwazo kwa kurudisha makubaliano ya kidemokrasia kutoka kwa Maduro, uliamua kutoa leseni na uidhinishaji ambao pia utairuhusu Caracas kuanza tena biashara na mataifa ya Caribean.
Serikali ya Venezuela na upinzani unaoungwa mkono na Marekani walifikia makubaliano juu ya kufanyika uchaguzi utakaofuatiliwa kimataifa katikati ya mwaka ujao. Hatua hiyo inaashiria hatua muhimu katika mabadiliko thabiti ya utawala wa Biden kuelekea kuimarika kwa ushirikiano na Venezuela.