MigogoroUkraine
Marekani kuipatia Ukraine msaada mpya wa dola mil. 225
7 Juni 2024Matangazo
Msaada huo mpya unatolewa wakati Rais Joe Biden akisisitiza tena kwamba wataendelea kuisaidia Ukraine na kamwe hawataruhusu Urusi kuitisha Ulaya.
Silaha hizo zitakatumiwa na vikosi vya Kyiv kushambulia ndani ya Urusi ili kuulinda mji wake wa Kharkiv unaoshambuliwa vikali na Urusi.
Alitoa hakikisho hilo katika hotuba ya jana Alhamisi mbele ya kaburi la Wamarekani kwenye eneo la Normandy wakati wa kumbukumbu ya miaka 80 ya D-Day.
Marekani hivi karibuni iliipa idhini Ukraine kutumia silaha zake kushambulia ndani ya Urusi na hii leo Biden anatarajiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Paris.