Marekani: Polisi ya Kenya kukabiliana na uhalifu Haiti
2 Agosti 2023Matangazo
Magenge hayo yanalidhibiti eneo kubwa la mji mkuu na yanasambaa kote katika taifa hilo la Caribbean. Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield amesema Marekani inaukaribisha uamuzi wa Kenya kuongoza kikosi hicho cha kimataifa. Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry alituma ombi la dharura Oktoba mwaka jana la kupelekwa haraka jeshi maalum, katika kiwango kinachofaa kuyakomesha magenge. Kenya ni nchi ya kwanza kuitikia wito huo, ikisema iko tayari kupeleka maafisa 1,000 wa polisi kusaidia kutoa mafunzo na kulisaidia jeshi la polisi la Haiti kurejesha utulivu nchini humo na kuyalinda maeneo ya kimkakati.