Marekani yaionya RSF dhidi ya kuishambulia Darfur
2 Novemba 2023Matangazo
Katika taarifa Blinken amesema hatua hiyo itawaweka watu hao katika hatari kubwa. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ametoa wito wa pande zinazozana kusitisha mashambulizi zaidi na kuwajibika chini ya sheria ya kimataifa ya kiutu kuhusu raia.
Ingawa Marekani haikutaja chanzo cha taarifa yake, taarifa hiyo inatiliwa maanani kwa kuwa imetoka kwa jina la Blinken.
Marekani yatiwa wasiwasi na mashambulizi ya RSF
Tangu mwezi Aprili, vita hivyo kati ya wanamgambo wa Rapid Support Forces RSF wanaoongozwa na Jenerali Mohamed hamdan Daglo, na vikosi vya jeshi la Sudan vilivyo chini ya mkuu wa nchi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 9 na kuwaacha watu milioni 5.6 bila makao.