1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Marekani yalisisitizia jeshi la Sudan kuhudhuria mazungumzo

15 Agosti 2024

Mazungumzo hayo yaliyoanza nchini Uswisi, yanahudhuriwa tu na wanamgambo wa RSF, kundi hasimu kwa jeshi la Sudan.

https://p.dw.com/p/4jUSz
Tom Perriello mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Sudan mjini Geneva
Tom Perriello mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Sudan mjini GenevaPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani Antony Blinken, kwa njia ya simu ametoa wito huo kwa kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abddel Fattah al-Burhan.

Msemaji wa wizara hiyo ya kigeni ya Marekani Vedant Patel amesema Blinken katika mazungumzo yake ya simu na al-Burhan, amemsisitizia umuhimu wa kushiriki kwake na haja ya pande zote mbili kusitisha mapigano na kuhakikisha mamilioni ya watu wanaotaabika wanafikiwa na misaada ya kiutu.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Sudan, Tom Perriello baada ya kikao cha ufunguzi alisema kwamba wakati umewadia sasa wa vita hivyo kufika mwisho.