SiasaMarekani
Marekani yarejea UNESCO baada ya kujitoa kwa miaka 6
1 Julai 2023Matangazo
Kikao maalum cha Baraza Kuu la UNESCO kimepiga kura kwa wingi kuijeresha Marekani ndani ya shirika hilo licha ya upinzani kutoka Urusi na China. Mataifa mengine yaliyopinga azimio hilo ni Iran, Syria, na Korea Kaskazini.
Soma zaidi:Marekani yajiondoa uanachama UNESCO
Rais wa zamani wa Marekani alioondoa rasmi nchini hiyo ndani ya UNESCO mnamo mwaka 2018 akilituhumu shirika hilo kuwa na chuki dhidi ya Israel.
Marekani ambayo ni moja ya wanachama waanzilishi wa shirika hilo ilikuwa mchangiaji mkubwa wa bajeti ya UNESCO hadi mwaka 2011 pale shirika hilo lilipoikaribisha Palestina uamuzi uliozusha ukosoaji kutoka Washington.