1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Israel haijajiandaa kuishambulia Rafah

9 Februari 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema jana kwamba taifa hilo halijaona ushahidi wowote kwamba Israel imejiandaa vya kutosha kuushambulia mji Rafah ulioko kusini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4cD94
Matokeo ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo la Rafah siku ya Ijumaa (9 Februari 2024).
Matokeo ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo la Rafah siku ya Ijumaa (9 Februari 2024).Picha: Doaa Albaz/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa wizara hiyo, Vedant Patel. amewaambia waandishi wa habari kwamba operesheni kama hii kwa wakati huu bila ya mipango katika eneo linalowahifadhi watu milioni moja itakuwa ni janga.

Soma zaidi: Blinken amaliza ziara ya Mashariki ya Kati baada ya Israel kukataa pendekezo la kusitisha vita

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Jumatano kwamba vikosi vya Israel vilikuwa vinajiandaa kuushambulia mji wa Rafah, ulioko kwenye mpaka na Misri.

Watu wengi wanaoishi kwenye mji huo waliyakimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza wakati Israel ikiendeleza mashambulizi yake ya dhidi ya wanamgambo wa Hamas.