1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Marekani yaahidi kuhamasisha msaada mkubwa kwa ajili ya Gaza

14 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken ametoa wito wa upelekwaji wa misaada mingi zaidi ya kibiaanadamu katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dUP9
Israel | Ramadhan
Randa Baker, kulia, aliyekimbia mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, akitayarisha Iftar na mama yake katika siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika hema ya muda iliyoko Muwasi, kusini mwa Gaza, Machi. 11, 2024.Picha: Fatima Shbair/AP/picture alliance

Blinken amesema amefanya mkutano kwa njia ya mtandao na maafisa wa Cyprus, Uingereza, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar na Umoja wa Ulaya kuanzisha njia mpya ya majini kwa ajili ya kuingiza misaada Gaza.

Amesema hatua hiyo itasaidia usambazaji wa chakula kwa Wapalestina hadi milioni mbili wanaoishi Ukanda wa Gaza uliozingirwa.

Blinken amesema njia hiyo ya baharini haitakuwa mbadala wa zile za nchi kavu na kuongeza kuwa suala la kunzishwa upya kwa njia hizo pia lilikuwa la kipaumbele.