1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatahadharisha uwezekano wa mashambulizi ya Urusi

22 Agosti 2024

Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv umetahadharisha juu ya uwezekano wa kufanyika mashambulizi ya makombora na droni za Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4jmTA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensk
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskPicha: Juan Carlos Rojas/picture alliance

Urusi inafanya mashambulizi hayo katika wakati ambapo nchi hiyo inapojiandaa kuadhimisha miaka 33 tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka Umoja wa Kisovieti.

Katika taarifa, ubalozi huo umesema kuna hatari inayoongezeka ya kutokea mashambulizi kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru wa Ukraine mnamo Agosti 24.Taarifa hiyo imechapishwa kwenye tovuti ya ubalozi wa Marekani jana jioni.

Soma pia:Urusi: Mashambulio ya droni kuilenga Moscow hayakufanikiwa
Kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskyi ameeleza mapema wiki hii kuwa Urusi imefanya mashambulizi ya makombora 9,600 na droni 14,000 tangu ilipoivamia Ukraine mnamo Februari 2022.