MigogoroSudan
Marekani yatoa nyongeza ya mamilioni ya dola kuisaidia Sudan
19 Julai 2024Matangazo
Licha ya msaada huo alioutangaza jana, Greenfield ameonya kuwa hilo siyo suluhisho la mzozo wa nchi hiyo.
Mwakilishi huyo wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amezitolea wito nchi wanachama, kutimiza ahadi zao kwa Sudan,inayokabiliwa na vita ili kushughulikia kile alichokiita mgogoro mbaya zaidi wa kiutu duniani.
Mwezi Aprili mwaka huu, viongozi wa dunia waliahidi kuichangia nchi hiyo zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 2.1, katika mkutano wa wahisani uliofanyika mjini Paris.
Sudan, iliingia katika machafuko mwezi Aprili mwaka 2023 baada ya kuibuka mivutano kati ya kiongozi wa jeshi rasmi la nchi hiyo Abdel Fattah al Burhan na kikosi cha wanamgambo wa RSF kinachoongozwa na Hamdan Dagalo.