1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatowa dola $5M kumpata kiongozi wa al-Shabaab

18 Oktoba 2023

Marekani imetoa ahadi ya zawadi ya dola milioni 5 kwa taarifa kuhusu kiongozi wa kundi la Al Shabaab nchini Somalia, Abukar Ali Adan.

https://p.dw.com/p/4Xfq5
Al-Schabaab Miliz in Somalia
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la al-Shabaab waliokamatwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Somalia.Picha: Tobin Jones/Au Un Ist/dpa/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Abukar Ali Adan, ambaye alitangazwa rasmi kama gaidi na Marekani mnamo 2018, ni naibu kamanda wa al-Shabaab na anahusishwa na matawi kadhaa ya mtandao wa kigaidi ya al-Qaida.

Wizara hiyo pia imesema kundi la Al Shabaab linaendelea kupanga na kufanya njama za vitendo vya kigaidi dhidi ya Marekani, maslahi ya Marekani na washirika wake wa kigeni.

Soma zaidi: Watu 35 wauawa kwenye mapigano kati ya jeshi na Al Shabaab

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kithure Kindiki ameapa vita kamili dhidi ya al-Shabaab na kutaja watu 35 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi hilo na waliohusika na mashambulizi katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia.