Marekani yatuma ndege za misaada ya kibinadamu Gaza
28 Novemba 2023Matangazo
Ndege hizo za kijeshi zilizobeba vyakula, vifaa vya matibabu na nguo nzito za majira ya baridi, ni msaada wa kwanza kutolewa na jeshi la Marekani tangu kuanza kwa mzozo kati ya Israel na Hamas Oktoba 7.
Msaada huo umetokea siku moja tu baada ya Rais Joe Biden kueleza kuwa, atatumia mwanya wa usitishwaji wa mapigano kupeleka misaada zaidi Gaza.
Soma pia:Mzozo wa Israel-Hamas: Mateka zaidi watarajiwa kuachiwa
Umoja wa Mataifa utauchukua msaadahuo wa Marekani kutoka eneo la Sinai kaskazini mwa Misri unaopakana na ukanda wa Gaza unaotawaliwana Hamas, na kuusafirisha hadi ndani ya mamlaka ya Palestine.
Ndege nyengine mbili za Marekani zilizobeba msaada zaidi zinatarajiwa kuwasili katika siku chache zijazo.