1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaweza kuvimaliza vita vya Ukraine - Kremlin

27 Januari 2023

Ikulu ya Urusi, Kremlin imesema kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden ana uwezo mkubwa wa kuumaliza mzozo wa Ukraine kwa kuielekeza Kiev, lakini hadi sasa hayuko tayari kuutumia.

https://p.dw.com/p/4MnrT
Russland Moskau | Wladimir Putin, Präsident
Picha: Aleksey Babushkin/Sputnik Kremlin/AP/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, wakati akizungumza na waandishi habari.

Mara kwa mara Urusi imekuwa ikiituhumu Marekani kwa kutoa maagizo kwa Ukraine na kuuzidisha mzozo kwa kuipatia Kiev silaha.

Soma zaidi: Urusi: Marekani haikutaka kuumaliza mzozo wa Ukraine

Marekani imesema Urusi imeanzisha vita vya kikatili na inaweza kuchagua kuvimaliza kwa kuwaondoa wanajeshi wake.

Urusi imesema vifaru aina ya Abrams vitakuwa ni sawa na kupoteza fedha kwa sababu wataviangamiza kama vifaru vingine vya Ukraine.